Header Ads Widget

Majeraha yamuondoa Hamza Stars

Beki wa Mashujaa Fc Ibrahim Ame ameitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuchukua nafasi ya Abdulrazak Hamza aliyepata majeraha

Hamza alikuwa sehemu ya wachezaji wa Simba waliokuwa wamejumuishwa kikosi cha Stars kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Afcon 2025 dhidi ya DR Congo

Ali Salim, Mohammed Hussein na Kibu Denis ni wachezaji wengine wa Simba walioko katika kikosi cha Stars

Hamza amekuwa katika kiwango bora tangu alipojiunga na Simba akijihakikishia nafasi kuanza katika kikosi cha kocha Fadlu Davids

Post a Comment

0 Comments