Header Ads Widget

Alicho kisema kocha mkuu wa simba baada ya kutoa sare na Coastal union leo

Simba imedondosha alama mbili uwanja wa KMC Complex leo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Unaweza kusema mlinda lango Moussa Camara leo alikuwa na siku mbaya kwani aliruhusu mabao mawili yanayofanana yote yakifungwa kutokea nje ya 18

Simba ilitangulia kufunga mabao yake mawili katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Mohammed Hussein na Lionel Ateba aliyefunga kupitia mkwaju wa penati

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema hayakuwa matokeo mazuri kwao kwani walikuwa na nafasi ya kushinda mchezo huo

"Tunacheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi lakini tunapaswa kuongeza ukatili mbele ya lango. Wapinzani wetu wamepata nafasi mbili na wamefunga mabao mawili, sisi tulipata nafasi nyingi zaidi hatukuzitumia ipasavyo"

"Tunarejea katika uwanja wa mazoezi kuboresha mapungufu yaliyojitokeza ili kuhakikisha haturudii makosa katika mchezo unaofuata dhidi ya Yanga," alisema Fadlu

Post a Comment

0 Comments